Jumatano 24 Desemba 2025 - 23:00
Njia ya mapambano ya Kiislamu inawezekana kwa kufuata mafundisho ya Qur’ani na Sunna

Hawza/ Rais wa Chuo Kikuu cha Ilya cha Iraq, katika kongamano la kimataifa la “Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah”, alisisitiza kuwa njia ya mapambano ya Kiislamu inawezekana tu kwa kushikamana na mafundisho ya Qur’ani Tukufu na Sunna ya Mtume pamoja na Maimamu watoharifu (a.s), na kwamba kizazi cha vijana kinapaswa kuendeleza njia yao ya uongofu wa kiroho na kijamii kwa kuiga mashahidi na viongozi wa mapambano.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Habari wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Mashhad, Sheikh Ghalib Abdulhussein Naeema, Rais wa Chuo Kikuu cha Ilya cha Iraq, leo Jumatano tarehe 24 December, katika kongamano la kielimu la kimataifa lenye anuani isemayo “Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah; alama ya muqawama na Umahiri katika Uongozi”, lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Kiislamu cha Razavi, alichambua vipengele mbalimbali vya uongozi na mapambano ya Kiislamu.

Akiashiria hadhi ya Ahlul-Bayt wa Mtume (saww), alisisitiza kwamba; uongozi wa jamii ya Kiislamu na uhifadhi wa maadili ya kidini katika historia yote umefanikishwa kwa uwepo wa Maimamu watoharifu. Naeema alisema kuwa; njia ya Qur’ani na Sunna ya Mtume daima imekuwa chanzo cha msukumo kwa viongozi na waumini, na imesababisha kuibuka kwa mapambano dhidi ya dhulma na ufisadi.

Akikumbusha nafasi ya Imam Ali bin Musa na Maimamu wengine katika uongozi wa kiroho kwa watu, alieleza kuwa: ukuaji wa kiroho wa binadamu umeambatana na uwepo na uongozi wa Maimamu na viongozi wa kimungu, na baraka pamoja na neema za Mwenyezi Mungu zimeendelea kumiminika katika njia hii.

Rais wa Chuo Kikuu cha Ilya cha Iraq kisha akarejea nafasi ya Shahidi Jenerali Qassem Suleimani na Sayyid Hassan Nasrallah katika muqawama wa Kiislamu, akisema: watu hawa ni vielelezo vya ujasiri, uono wa mbali na umahiri wa uongozi, ambao kwa kufuata misingi ya Qur’ani na ya kimungu waliweza kusimama imara dhidi ya dhulma na uvamizi.

Aliongeza kuwa: mafanikio katika njia ya muqawama yanawezekana tu kwa kushikamana na maadili ya kimungu na kunufaika na mafundisho ya Qur’ani na Sunna; uzembe wowote, kushindwa au kosa lolote linaweza kuigharimu jamii ya Kiislamu gharama kubwa.

Sheikh Naeema, akisisitiza umuhimu wa kuijua historia na kujifunza kutoka katika maisha ya viongozi na mashahidi, alisema: kizazi cha vijana kinapaswa kwa kusoma kwa kina maisha na utendaji wa watu hawa, kuitambua njia sahihi ya uongofu na muqawama na kuiga mwenendo wao; kuzingatia mafundisho ya kimaadili na kidini, kuifahamu kwa undani historia na kunufaika na miongozo ya Qur’ani, kunaweza kuifanya jamii iwe imara dhidi ya fitina na changamoto za ndani na nje.

Rais wa Chuo Kikuu cha Ilya cha Iraq pia aliitaja nafasi ya elimu na maarifa katika kuimarisha imani na muqawama, na akaendelea kusema: walimu na wahadhiri wana jukumu muhimu katika kuhamisha maadili ya kidini na kimaadili kwa wanafunzi na kizazi cha vijana, na wanapaswa kwa kutoa miongozo sahihi kuweka mazingira ya ukuaji wao wa kiroho na kijamii.

Alisema kuwa: elimu, inapokuwa pamoja na imani, humwezesha mwanadamu kutofautisha njia sahihi na makosa, badala ya kufuata upofu, hutenda kwa uono wa mbali na uelewa.

Sheikh Naeema alisisitiza juu ya kuendelea kwa muqawama, kushikamana na maadili ya kimungu na umuhimu wa kuwaongoza watu kwa uongofu sahihi, akasema: kuiga mashahidi na viongozi wa muqawama, hususan Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, kunaweza kuwaongoza vijana katika njia ya ukuaji wa kiroho na kijamii na kusababisha kuendelea kwa harakati ya muqawama wa Kiislamu duniani.

Aliongeza kuwa: kizazi cha vijana kinapaswa kwa kupata msukumo kutoka katika kujitolea, ujasiri na mtazamo wa mbali wa watu hawa, kuyatekeleza maelekezo ya kidini na kimaadili katika maisha yao, ili jamii ya Kiislamu iendelee kubakia thabiti na imara.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha